HomeBiasharaAirtel yasogeza suluhisho za kidijitali Maonesho ya Tano ya SIDO Kahama

Airtel yasogeza suluhisho za kidijitali Maonesho ya Tano ya SIDO Kahama

Kahama, 24 Oktoba 2026. Airtel Tanzania, kupitia kitengo cha huduma kwa biashara, yasogeza suluhisho za kidijitali na mawasiliano zinazolenga kusaidia wafanyabiashara katika Maonesho ya Kitaifa ya Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), yanayofanyika katika Viwanja vya Magufuli, Manispaa ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga, kuanzia Oktoba 21 hadi 30, 2026.

Maonesho hayo ya siku 10 yameandaliwa na Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, yakishirikisha zaidi ya wajasiriamali na wafanyabiashara ndogondogo zaidi ya 600 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

Akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa maonesho hayo, Judith Kapinga, Waziri wa Viwanda na Biashara, alieleza juhudi za Serikali za kupanua wigo wa upatikanaji wa mikopo kwa wajasiriamali ili kuwawezesha kukuza biashara zao, kuongeza uzalishaji na kutengeneza ajira. Pia alihimiza ushirikiano zaidi kati ya taasisi binafsi na SIDO katika kutafuta njia za kukabiliana na changamoto mbalimbali.

“Lengo la Serikali hii ya Awamu ya Sita ni kuhakikisha huduma hizi zinaendelea kuwafikia wajasiriamali wengi zaidi, hasa wale wenye uwezo wa kuzalisha na kukuza biashara lakini wanaokabiliwa na vikwazo vya kupata fedha za mitaji. Nitumie pia fursa hii kuzihimiza taasisi za fedha kuendelea kushirikiana na Serikali kupitia SIDO katika kubuni huduma zinazozingatia mahitaji ya wajasiriamali wadogo na wa kati ili kuendeleza sekta hii nchini,” alisema.

Waziri Kapinga pia aliitaka SIDO kuelekeza mikopo zaidi katika shughuli za uzalishaji na uongezaji thamani wa bidhaa, hatua inayoweza kuimarisha viwanda vya ndani na kuongeza fursa za ajira.

Kwa upande wake, Joseph Vipond, Mkurugenzi wa Airtel Business, alisema ushiriki wa Airtel Tanzania katika maonesho hayo unaonesha dhamira yake ya kuwasaidia wafanyabiashara kupata suluhisho za kidijitali zinazoweza kuboresha shughuli zao na kusaidia ukuaji wa biashara.

“Biashara ndogo na za kati ni nguzo muhimu ya uchumi wa Tanzania. Ushiriki wetu katika Maonesho ya Kitaifa ya SIDO unaonesha dhamira yetu ya kuwasogezea wafanyabiashara suluhisho za kidijitali zilizo nafuu, za kuaminika na zinazokidhi mahitaji yao. Kupitia huduma kama Airtel Chapakazi na SME Bundles, tunasaidia biashara kudhibiti gharama za mawasiliano, kuongeza ufanisi wa shughuli zao na kuzingatia kukuza biashara na kuwahudumia wateja,” alisema.

Suluhisho zilizoangaziwa ni pamoja na:

  • Airtel Chapakazi ni suluhisho la kidijitali linalojumuisha data (intaneti), dakika za maongezi na SMS kwa gharama nafuu, maalum kwa ajili ya wajasiriamali na biashara ndogo na za kati (SMEs). Vifurushi hivi vinawawezesha wafanyakazi wanaotekeleza majukumu yao nje ya ofisi kuwasiliana na wateja pamoja na wenzao kwa urahisi na unafuu mkubwa zaidi.
  • Vifurushi vya Airtel SME na Corporate Yatosha vinatoa suluhisho mseto la mawasiliano kupitia mifumo ya malipo ya baada ya matumizi (postpaid) na mipango mseto (hybrid). Huduma hii inajumuisha vifurushi vya data vinavyoweza kugawanywa miongoni mwa watumiaji (data rollover/pooling), pamoja na mfumo wa mawasiliano ya ndani ya kikundi (Closed User Group – CUG) unaowezesha wafanyakazi kupigiana simu bila kikomo na bure. Suluhisho hizi zimeundwa mahususi kusaidia makampuni kudhibiti gharama za uendeshaji na kurahisisha mawasiliano ya timu.
  • Airtel SmartConnect na Pocket Wi-Fi: Suluhisho za intaneti ya kasi kupitia teknolojia za 4G/5G, zinazosaidia biashara kuunganishwa na intaneti ofisini na wanapokuwa safarini. Ina vifaa vyenye betri ya akiba ambavyo vinasaidia upatikanaji wa intaneti pale umeme unapokatika, kulingana na uwezo wa kifaa husika na upatikanaji wa mtandao.
  • Airtel Money Enterprise Services: Suluhisho la malipo ya kidijitali inayowezesha biashara kufanya miamala kwa urahisi na usalama, ikiwemo malipo ya mishahara, pamoja na ukusanyaji wa malipo kutoka kwa wateja kupitia namba za Till na QR.

Kupitia ushiriki wake katika maonyesho haya, Airtel Tanzania inaendelea kudhihirisha dhamira yake ya kuchangia ukuaji wa uchumi wa Taifa. Airtel inafanya hivyo kwa kuwezesha ustawi wa biashara ndogo na za kati nchini kupitia suluhisho za mawasiliano na kidijitali. Suluhisho za mawasiliano ya kidijitali zinazowawezesha wafanyabiashara kuwasiliana na kuwafikia wateja wao kiurahisi zaidi, kushindana katika soko na kukuza biashara zao.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments