HomeAfyaIreland, Amref kushirikiana kuimarisha huduma za afya Tanzania

Ireland, Amref kushirikiana kuimarisha huduma za afya Tanzania

Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Nicola Brennan, amesema nchi hiyo itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania pamoja na wadau wa maendeleo katika kuimarisha huduma za afya na kukuza maendeleo endelevu ya jamii, akitaja wanawake, wasichana na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kuwa miongoni mwa maeneo yatakayopewa kipaumbele.

Brennan ametoa kauli hiyo Oktoba 19, 2026, alipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dk. Batilda Burian, na kueleza kuwa mkakati mpya wa Ireland nchini Tanzania utazingatia vipaumbele vya maendeleo vya Serikali.

Amesema ushirikiano huo utahusisha Serikali na wadau wa maendeleo, wakiwemo Amref Health Africa Tanzania, kwa lengo la kuimarisha huduma za afya na kuchangia mabadiliko chanya katika jamii.

Kwa upande wake, Dk. Batilda amesema ukuaji wa uchumi wa Mkoa wa Tanga unachangiwa na sekta mbalimbali, zikiwemo afya na kilimo.

Amesisitiza umuhimu wa ushirikiano na wadau wa maendeleo katika kuendeleza sekta hizo na kuboresha maisha ya wananchi.

Ireland inaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania na wadau mbalimbali katika juhudi za kuimarisha huduma za afya na kukuza maendeleo endelevu ya jamii.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments