HomeBiasharaEWURA yataka watumishi kuongeza ufanisi wa huduma za kiudhibiti

EWURA yataka watumishi kuongeza ufanisi wa huduma za kiudhibiti

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Salum Mnuna, amewataka watumishi wa mamlaka hiyo kuendelea kuongeza ufanisi katika utendaji na utoaji wa huduma za kiudhibiti ili kuleta matokeo chanya kwa wadau na wananchi.

Mnuna ametoa wito huo leo, Novemba 11, 2026, mjini Singida, wakati akifungua kikao cha kwanza cha Baraza la Tatu la Wafanyakazi wa EWURA.

Amesema mamlaka hiyo inaendelea kuweka mazingira wezeshi yatakayovutia sekta binafsi kushiriki katika utoaji wa huduma zinazodhibitiwa, huku ikiimarisha matumizi ya nishati safi ya kupikia na utendaji wa mamlaka za maji nchini.

Ameongeza kuwa EWURA pia inaendelea kutekeleza Mpango Kabambe wa Taifa wa Nishati, ambao ni sehemu ya juhudi za kuimarisha upatikanaji na utoaji wa huduma za nishati.

Aidha, amesema mamlaka hiyo inatumia mbinu zenye ufanisi na teknolojia katika shughuli zake za udhibiti, ikiwemo kuimarisha mifumo ya kidijitali ili kuboresha utoaji wa huduma na kulinda maslahi ya wawekezaji, watoa huduma na watumiaji.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments