HomeBiasharaChalinze yatenga Sh bilioni 1.3 kwa miradi ya maendeleo

Chalinze yatenga Sh bilioni 1.3 kwa miradi ya maendeleo

Shilingi Billioni 1.3 zimetokewa na Halamshauri ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027.

Hayo ni kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Leon Mgweno, alipokuwa akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika Novemba 12.

Mgweno amesema fedha hizo zimepokelekwa katika kata kwa ajili ya kutekelza miradi mbalimbali ikiwemo ya elimu ambayo inakwenda kuleta mabadiliko ya kiuchumi katika Halmashauri hiyo.

“Ilielekezwa kujenga eneo la maegesho ya malori na sasa linaendelea utekelezaji wake, soko la wajasiriamali tumeshatangaza mzabuni muda wowote kuanzia sasa wafanyabiashara wetu watapata sehemu nzuri yenye miundombinu rafiki kwa ajili ya kufanyia biashara zao,” amesema.

Mwenyekiti huyo amepongeza ongezeko la makusanyo ya mapato, ambapo amesema hali hiyo inachangia kutekeleza miradi ya maendeleo katika Halmashauri hiyo.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abubakar Mlawa amesema ongezeko la ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri hiyo, linatakiwa kuwa chachu ya maendeleo ikiwa ni pamoja na uwepo wa miradi iliyokamilika yenye kuwasaidia wananchi.

” Fedha zinazokusanywa zikamalizie maboma yaliyoanzishwa, lakini pia wataalamu wetu jengeni tabia ya kukutana na hawa wawekezaji mkawaeleweshe namna ya kuchangia kwenye jamii,” amesema.

Mlawa pia amewataka Madiwani kushuka kwa wananchi kusikiliza kero zao na kutafuta namna ya kuzitatua badala ya kusubiri viongozi wa ngazi za juu kufika kuwasikiliza.

Katika kikao hicho Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Ramadhani Possi ameombwa kusaidia ukarabati wa barabara inayoelekea katika chuo cha ufundi ili iweze kupitika wakati wote.

Wakati huo huo Diwani wa Miono Fransis Kilo, ameiomba Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kusaidia upatikanaji wa maji kuwaondolea kero inayowakabili wakazi wa Kweikonje.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments