HomeHabariRais Samia: Tumeongeza kasi matumizi nishati safi ya kupikia

Rais Samia: Tumeongeza kasi matumizi nishati safi ya kupikia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali inalenga kuhakikisha asilimia 35 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwishoni mwa mwaka 2026, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kulinda afya za wananchi na mazingira.

Amesema upatikanaji wa nishati safi ya kupikia nchini umeongezeka kutoka asilimia 16 mwaka 2022 hadi asilimia 28.26 Machi 2024, huku gesi asilia ikichangia asilimia 61 ya uzalishaji wa umeme nchini.

Rais Samia ameyasema hayo leo, Novemba 12, 2026, katika Mkutano wa Ngazi ya Juu kuhusu Nishati Safi ya Kupikia Barani Afrika, uliofanyika pembezoni mwa Mkutano wa 31 wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP31), Antalya, Uturuki.

“Maendeleo haya yamechangiwa na hatua mbalimbali zinazotekelezwa na Serikali, zikiwemo kuimarisha elimu kwa umma, kupunguza gharama za umeme unaotumika kupikia, kutoa ruzuku kwa vifaa vya gesi ya mitungi (LPG) na kutoa vivutio kwa teknolojia za nishati safi ya kupikia,” amesema Rais Samia. #TanzaniaCOP31

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments