HomeHabariMalagarasi kuimarisha huduma ya umeme mikoa ya Magharibi

Malagarasi kuimarisha huduma ya umeme mikoa ya Magharibi

UPATIKANAJI wa umeme wa uhakika ni miongoni mwa mahitaji muhimu kwa wananchi na biashara, kwani huwezesha shughuli za uzalishaji, kuongeza fursa za uwekezaji na kuboresha huduma zinazotegemea nishati hiyo.

Matarajio hayo yanaelekezwa katika Mradi wa Kufua Umeme kwa Maji wa Malagarasi, mkoani Kigoma, unaotekelezwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), ambao utakapokamilika unatarajiwa kuzalisha megawati 49.5.

Umeme utakaotokana na mradi huo unatarajiwa kuimarisha upatikanaji wa nishati katika Mkoa wa Kigoma na maeneo mengine ya Magharibi mwa Tanzania, hatua inayoweza kusaidia biashara, viwanda na shughuli mbalimbali za uzalishaji.

Aidha, upatikanaji wa umeme wa uhakika unaweza kuongeza mvuto wa maeneo hayo kwa wawekezaji, kupunguza changamoto za nishati kwa wajasiriamali na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments