HomeHabariVijana kuwa sehemu ya suluhisho la mabadiliko ya tabianchi

Vijana kuwa sehemu ya suluhisho la mabadiliko ya tabianchi

Benki ya CRDB imeendelea kuonesha dhamira yake ya kuwawezesha vijana kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, kwa kupanua fursa za upatikanaji wa mitaji, elimu na ushirikiano utakaowawezesha kubadili mawazo bunifu kuwa biashara endelevu, ajira za kijani na suluhisho zenye manufaa kwa jamii.

Dhamira hiyo imeelezwa na Meneja wa Uhusiano wa Taasisi za Kimataifa wa Benki ya CRDB, Terence Mponjoli, wakati akishiriki mjadala kuhusu ufadhili wa biashara zinazoongozwa na vijana katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa haki na kuimarisha ustahimilivu wa jamii, uliofanyika pembezoni mwa Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP31) jijini Antalya, Türkiye.

Amesema Benki ya CRDB, ikiwa taasisi ya fedha pekee nchini Tanzania yenye ithibati ya Mfuko wa Kimataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (GCF), inaendelea kuwekeza katika suluhisho za kifedha zinazochochea maendeleo endelevu, ikiwemo programu ya Dola za Marekani milioni 200 ya kuimarisha ustahimilivu wa sekta ya kilimo dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi.

Aidha, kupitia taasisi yake ya CRDB Bank Foundation na mpango wa Go Green na iMBEJU, Benki inaendelea kuwawezesha vijana na wanawake kupata mitaji, mafunzo na fursa za kuanzisha na kukuza biashara zinazolinda mazingira na kuchochea uchumi wa kijani.

Ushiriki wa Benki ya CRDB katika COP31 unaendeleza jitihada zake za kujenga ushirikiano wa kimataifa na kufungua fursa zaidi za ufadhili wa miradi bunifu inayowawezesha vijana kuwa sehemu ya suluhisho la changamoto za mabadiliko ya tabianchi.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments