HomeBiasharaDC Nkurlu ataka vijana kutumia vizuri Programu ya BBT

DC Nkurlu ataka vijana kutumia vizuri Programu ya BBT

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Fadhil Nkurlu, amewataka vijana wanufaika wa Programu ya Jenga kesho Iliyo Bora (BBT) kutumia fursa hiyo kujikwamua kiuchumi.

Nkurlu ameyasema hayo alipokuwa akizindua shughuli ya ugawaji wa maeneo kwa ajili ya utekelezaji wa programu hiyo na kukabidhi mikataba kwa wanufaika,

Mkuu huyo wa wilaya amesema, ardhi na kilimo ni biashara, uwekezaji na chanzo cha utajiri, hivyo vijana hao wanatakiwa kutumia vizuri fursa waliyoipata.

Naye Mkuu wa Idara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo wa Halmashauri hiyo, Zahoro Thabiti, amesema maombi 502 kwa ajili ya utekelezaji wa programu hiyo yalipokelewa, ambapo vijana 229 walikidhi vigezo, wakiwemo wanawake 115 na wanaume 114.

Amesema kati ya ekari 300 zilizotengwa, ekari 250 zitatumika kwa shughuli za kilimo na ekari 50 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali, huku maandalizi ya awali ya mradi huo yakigharimu Sh milioni 165.6.

Kwa upande wake, Muhidin Semgonde wa timu ya uratibu BBT kutoka Wizara ya Kilimo amesema serikali imechagua vijana 2,960 kunufaika na awamu ya pili ya BBT kupitia mashamba ya pamoja.

Amesma, serikali imetambua hekari 136,216 nchi nzima kwa ajili ya mashamba ya pamoja sawa na asilimia 40 ya lengo la hekari 340,000 lililowekwa katika kipindi cha utekelezaji wa mradi.

Vijana 229, katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, wamenufaika na mpango wa ugawaji ardhi kwa ajili ya Programu hitting ambapo kila mmoja atapata ekari moja katika ardhi hiyo yenye ukubwa wa ekari 300 iliyopo Kata ya Kikongo.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments