Novemba 18, 2026 – Cape Town, Afrika Kusini: Qualcomm Technologies, Inc. leo imetangaza kuhitimishwa kwa programu yake ya nne ya kila mwaka ya ‘Qualcomm Make in Africa Startup Mentorship Program’, iliyofikia kilele chake kupitia hafla ya kwanza iliyofanyika ana kwa ana katika maonyesho ya ‘Africa Tech Festival’ jijini Cape Town. Qualcomm pia imetangaza mshindi wa Mfuko wa Uwekezaji wenye Matokeo kwa Kijamii wa ‘Qualcomm for Good Social Impact Fund’ wa mwaka 2026.
Mambo muhimu:
- Programu ya mwaka 2026 ilisaidia kampuni changa kumi (startups) kutoka nchi tisa za Afrika (kampuni ya SafeSip ya Tanzania inayotoa suluhisho la maji salama linalotumia teknolojia janja kwa maeneo ya mijini na pembezoni mwa miji ilikuwa miongoni mwao), zinazotengeneza suluhisho zinazotumia akili mnemba (AI) inayounganishwa na mifumo halisi (embodied AI) na teknolojia ya kompyuta inayochakata taarifa karibu na chanzo chake (edge computing), katika sekta za kilimo, ufugaji wa samaki, usafiri wa kielektroniki, usafishaji wa maji na upatikanaji wa huduma kwa watu wenye mahitaji maalum.
- Qualikeeper Investments Ltd (Zambia) imechaguliwa kuwa mshindi wa Mfuko wa Uwekezaji wenye Matokeo ya Kijamii wa ‘Qualcomm for Good Social Impact Fund’ wa mwaka 2026, kwa kutambua mfumo wake wa bei nafuu wa kidijitali unaounganisha akili mnemba na vifaa vya intaneti ya vitu (Edge-AIoT) kwa ajili ya ufuatiliaji na usimamizi wa mifugo, unaojulikana kama ‘StocKeeper’.
- Maombi ya kujiunga na programu ya Qualcomm Make in Africa ya mwaka 2027 yamefunguliwa. Waombaji wanaweza kutembelea tovuti ya Qualcomm ili kutuma maombi.
Kilele cha Hafla hiyo kiliwakutanisha washiriki wa programu ya mwaka 2026 jijini Cape Town, ambapo waanzilishi wa kampuni hizo kutoka maeneo mbalimbali barani Afrika waliwasilisha kazi zao kama hitimisho la programu hiyo. Suluhisho zao zinahusisha teknolojia za ‘embodied AI’ na ‘edge computing’, zilizotengenezwa kwa kutumia teknolojia za Qualcomm na jukwaa la maendeleo la Arduino.
Programu hii, ambayo haihitaji washiriki kutoa hisa za kampuni zao, inalenga kusaidia kampuni changa za teknolojia barani Afrika kupitia mafunzo ya biashara, msaada wa kiuhandisi na mwongozo kuhusu haki miliki. Washiriki wa mwaka 2026 walifanya kazi kwa kutumia teknolojia za Qualcomm® na jukwaa la maendeleo la Arduino®, ikiwemo Arduino® UNO™ Q.
Kupitia L2Pro Africa na ushauri wa kitaalamu kutoka Adams & Adams, washiriki walipata msaada wa vitendo katika kulinda na kufanya ubunifu wao kuwa bidhaa au huduma zinazoweza kuuzwa kibiashara. Baada ya kukamilika kwa programu, kampuni hizo pia zitapokea fedha za kusaidia shughuli zao kiasi cha dola za Marekani 5,000, pamoja na kurejeshewa gharama za mpaka dola za Marekani 5,000 kwa ajili ya maombi kamili ya mara moja ya cheti cha matumizi (utility patent).
“Programu ya Qualcomm Make in Africa inaakisi utabiti wa mifumo ya ubunifu na uvumbuzi inayokua barani Afrika, pamoja na uwezo mkubwa na mafanikio ya kipekee ya wajasiriamali wake,” alisema Wassim Chourbaji, Makamu wa Rais Mwandamizi na Rais wa Qualcomm kwa Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika (EMEA), Qualcomm France S.A.R.L.

“Kwa kuwapatia fursa ya kutumia teknolojia za Qualcomm, jukwaa la maendeleo la Arduino, ushauri na msaada kutoka katika mfumo wa wadau wa teknolojia na ubunifu, tunawasaidia waanzilishi wa kampuni kubadilisha mawazo bunifu na yenye maono makubwa kuwa suluhisho zinazounganishwa na mifumo halisi zinazoweza kupanuliwa na kuleta matokeo halisi kwa jamii, kwa ufanisi na gharama nafuu za matumizi ya nishati. Kupitia Mfuko wa Uwekezaji wenye Matokeo kwa Kijamii, tunajivunia kuunga mkono kampuni changa ambayo ubunifu wake unaonesha uwezo mkubwa wa kuboresha maisha na kuleta manufaa endelevu kwa kijamii na kiuchumi barani Afrika.”
“Kampuni changa kumi zilizoshiriki katika programu ya Qualcomm Make in Africa ya mwaka huu zinaonesha namna kujifunza mashine na teknolojia halisi zinavyoweza kutumika kutatua changamoto kwa vitendo katika sekta mbalimbali,” alisema Sudeepto Roy, Makamu wa Rais wa Uhandisi, Qualcomm Incorporated.
“Katika kipindi chote cha programu, kampuni hizo zimeendeleza mifumo yao ya majaribio huku zikijenga uelewa mpana zaidi kuhusu haki miliki na hatua zinazohitajika kuanzia uvumbuzi mpaka kufanikisha biashara. Maendeleo yao ni mfano wa kutia moyo unaoonesha vipaji vya kiteknolojia na ari ya ujasiriamali vinavyoibuka katika maeneo mbalimbali ya Afrika.”
Washirika kutoka serikalini na sekta binafsi pia walisisitiza umuhimu wa programu hiyo katika kuendeleza upatikanaji wa mawasiliano na uvumbuzi wa ndani barani Afrika.
“Kupitia Azimio la Abuja la mwaka 2026 kuhusu Upatikanaji wa Mawasiliano Yenye Tija kwa Afrika (2026 Abuja Declaration on Meaningful Connectivity for Africa), nchi wanachama wa Umoja wa Mawasiliano wa Afrika (ATU) zimethibitisha tena dhamira yao ya pamoja ya kuharakisha ujumuishaji wa kidijitali na kuhakikisha kuwa Waafrika wote wanapata fursa ya kushiriki kikamilifu katika uchumi wa kidijitali.
“Wabunifu waliochaguliwa kushiriki katika programu ya Qualcomm Make in Africa ya mwaka huu wanaonesha jinsi dira hii inavyoweza kutafsiriwa kuwa matokeo halisi, kwa kutumia akili mnemba, mawasiliano ya kisasa na teknolojia nyingine zinazoibuka kutengeneza suluhisho zinazokidhi mahitaji ya ndani, zinazoshughulikia changamoto halisi na kuboresha maisha ya jamii za Afrika,” alisema Martial Dhossa, Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Redio, Umoja wa Mawasiliano wa Afrika (African Telecommunications Union – ATU).

Mshindi wa Mfuko wa Uwekezaji wenye Matokeo ya Kijamii wa Qualcomm for Good Social Impact Fund
Mfuko wa Uwekezaji wenye Matoke ya Kijamii wa Qualcomm for Good hutoa ruzuku kwa kampuni moja changa kutoka kila kundi la washiriki wa Qualcomm Make in Africa, ili kusaidia suluhisho lenye uwezo mkubwa wa kuleta manufaa ya kijamii. Ruzuku hiyo husaidia kampuni kuendeleza na kusambaza suluhisho lake, kupima athari zake na kuongeza wigo wa utekelezaji wake.
Qualikeeper imetangazwa kuwa mshindi wa Mfuko wa Uwekezaji wenye Matokeo ya Kijamii wa Qualcomm for Good wa mwaka 2026. Kampuni hiyo itapokea ruzuku ya dola za Marekani 75,000 (zaidi ya Shilingi milioni 190 za Kitanzania) ambayo haihitaji kutoa hisa za kampuni, pamoja na msaada maalum wa kiufundi ili kusaidia kupanua suluhisho lake na kuongeza manufaa yake.
“Qualikeeper imechaguliwa kwa kutambua maono yake, ubunifu na dhamira yake ya kuimarisha afya ya mifugo na maisha ya wafugaji katika jamii zinazotegemea mifugo, hususan katika mazingira yenye rasilimali chache.
“Kwa kuunganisha ubunifu wa kiteknolojia na msisitizo wa kuleta matokeo halisi, timu hiyo inaonesha uwezo wa ujasiriamali wa Afrika katika kushughulikia changamoto muhimu na kuleta thamani endelevu kwa jamii,” alisema Erica Ciaraldi, Meneja wa Masuala ya Serikali, Qualcomm Incorporated.
“Tunafurahi kutambua mafanikio yao kupitia Mfuko wa Uwekezaji wenye Matokeo ya Kijamii wa Qualcomm for Good. Tunatarajia kuona namna watakavyoendelea kukuza mfumo wao wa teknolojia jumuishi wa akili mnemba (AIoT) wa ufuatiliaji wa mifugo, kufikia jamii mpya na kupanua manufaa yao barani Afrika na maeneo mengine duniani.”

Mwelekeo wa Baadaye: Programu ya Qualcomm Make in Africa Startup Mentorship Program 2027
Kwa kuendeleza mafanikio ya programu hiyo, maombi ya kujiunga na Qualcomm Make in Africa Startup Mentorship Program ya mwaka 2027 sasa yamefunguliwa.
Taarifa zaidi na maelezo ya namna ya kutuma maombi yanapatikana kupitia: https://www.qualcomm.com/
Kuhusu Qualcomm
Qualcomm inaendelea kufanya ubunifu wa kiteknolojia kwa lengo la kuwezesha mifumo ya kompyuta erevu kutumika kila mahali, kusaidia dunia kukabiliana na baadhi ya changamoto zake muhimu zaidi. Kwa kuendeleza uzoefu wake wa miaka 40 katika uongozi wa teknolojia na kuleta ubunifu unaobadilisha zama, kampuni inatoa wigo mpana wa suluhisho zinazotumia teknolojia zake za kisasa za akili mnemba, mifumo ya kompyuta yenye utendaji wa juu na matumizi madogo ya nishati, pamoja na uwezo wa kipekee wa mawasiliano.
Majukwaa ya Snapdragon® yanawezesha uzoefu wa kipekee kwa watumiaji, huku bidhaa za Qualcomm Dragonwing™ zikisaidia biashara na sekta mbalimbali kufikia viwango vipya vya ukuaji na mafanikio. Kwa kushirikiana na wadau wake katika mfumo wa teknolojia, Qualcomm inawezesha mabadiliko ya kidijitali ya kizazi kijacho ili kuboresha maisha, kuimarisha biashara na kuendeleza jamii.
Qualcomm Incorporated inajumuisha biashara yake ya utoaji leseni, QTL, pamoja na sehemu kubwa ya jukwaa lake la haki miliki. Qualcomm Technologies, Inc., kampuni tanzu ya Qualcomm Incorporated, pamoja na kampuni zake tanzu, husimamia takribani shughuli zote za uhandisi na utafiti na maendeleo, pamoja na sehemu kubwa ya biashara zake za bidhaa na huduma, ikiwemo biashara ya semikondakta ya QCT.
Bidhaa zenye chapa ya Snapdragon na Qualcomm ni bidhaa za Qualcomm Technologies, Inc. na/au kampuni zake tanzu. Teknolojia zilizo na cheti cha matumizi za Qualcomm zinatolewa kwa leseni na Qualcomm Incorporated. Qualcomm na Wireless Reach ni chapa za biashara au chapa za biashara zilizosajiliwa za Qualcomm Incorporated.
Qualcomm, Snapdragon na Qualcomm Dragonwing ni chapa za biashara au chapa za biashara zilizosajiliwa za Qualcomm Incorporated. Arduino ni chapa ya biashara au chapa ya biashara iliyosajiliwa ya Arduino S.r.l.




