Tuesday, March 3, 2026
spot_img
HomeHabariDk. Samia: Hatuna wasiwasi, tutatekeleza

Dk. Samia: Hatuna wasiwasi, tutatekeleza

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa hakikisho la kuendelea kutoa ruzuku za pembejeo na mbolea kwa mazao yote ikiwemo tumbaku ambalo ndilo zao kuu mkoani Tabora.

Sambamba na hilo, amesema hana wasiwasi wa kutekeleza ahadi anazotoa kwa kuwa alishaonyesha mfano katika miaka mitano iliyopita, hivyo Watanzania wampe nafasi ili kuinua utu na heshima kwa Mtanzania.

Dkt Samia ametoa kauli hiyo leo, Alhamisi Septemba 11, 2025 alipozungumza na wananchi wa Kaliua mkoani Tabora, katika mwendelezo wa kampeni zake za urais, zilizohudhuriwa na maelfu ya wananchi.

“Kwa upande wetu hatuna wasiwasi wa kuyatekeleza kwa sababu tulishatoa mfano, miaka mitano iliyopita tumetekeleza na mmeona na mbele hapo tutakwenda kutekeleza, ili kuinua utu na heshima kwa Mtanzania,” amesema.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments