HomeHabariBalozi CP Kaganda akemea vitendo vya ukatili wa kijinsia

Balozi CP Kaganda akemea vitendo vya ukatili wa kijinsia

Balozi wa Tanzania Nchini Zimbambwe, Kamishina wa Polisi (CP) Suzan Kaganda ameongoza zoezi la harambee ya kuchangia ukarabati wa kanisa la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Magharibi kati Jimbo la Mashariki, Usharika wa Ndala lilopo Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora.

Harambee hiyo imefanyika Oktoba 26,2026 katika Kanisa la KKKT lilolopo kata ya Ndala, kwa lengo la kufanya ukarabati mkubwa wa kuezeka paa jipya katika kanisa hilo pamoja na kuboresha muonekano wa mazingira ya ndani na nje ya nyumba hiyo ya Ibaada.

ameongoza kuwa Jamii inapaswa kuendelea kuwalea watoto katika misingi ya dini, na kuwalinda dhidi ya vitendo vya ukatili vya ukatili wa kijinsia.

Aidha amebainisha kuwa jamii inapaswa kumrudia Mungu na kuendelea kuliombea taifa na viongozi wake ili waendele kuwa ongoza vyema wananchi wake katika roho na kweli.

Kwa upande wake mwakilishili wa kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Mkuu wa Kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Tabora, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Peter Magayane amewataka wazazi na walezi kutoa taarifa za haraka dhidi ya matukio ya ukatili wa kijinsia ili hatua sitahiki za kisheria zichukuliwe.

Katika harambee hiyo, zaidi ya shilingi Millioni 70 zimechangishwa na Balozi CP Kaganda huku Mwakilishi wa Askofu Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Magharibi kati Mchungaji Patrick Katembo akishukuru kwa namna walivyoshikwa mkono wakiahidi kanisa hilo kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kudumisha amani na kukabiliana na vitendo vya uhalifu.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments