HomeHabariMpina asema hukumu ya Lissu kuleta sura mpya ya siasa

Mpina asema hukumu ya Lissu kuleta sura mpya ya siasa

Naibu Waziri Mkuu Kivuli wa ACT Wazalendo, Luhaga Mpina, amedai uamuzi wa kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, unaotarajiwa kutolewa kesho, unaweza kuwa na athari kubwa katika mwelekeo wa siasa za Tanzania.

Mpina amedai anaamini Lissu amekuwa akishikiliwa kwa kuonewa na kukabiliwa na mashtaka anayoyataja kuwa ya uongo, huku akieleza matumaini yake kuwa Mwenyezi Mungu atamsaidia kupata haki katika uamuzi huo.

Amesema yeye pamoja na Watanzania wengine wanamuombea Lissu ili aweze kupata haki na kushinda kile anachokitaja kuwa ni dhuluma na uonevu anaofanyiwa.

“Uamuzi wa kesi hiyo utaleta sura mpya ya siasa ndani ya nchi yetu. Naamini na pasipo mashaka kabisa Mheshimiwa Tundu Lissu amekaa ndani kwa kuonewa, amefunguliwa kesi za uongo,” amesema Mpina.

Aidha, Mpina amesisitiza kuwa maombi yake kwa Lissu yanatokana na umuhimu wa haki kwa mustakabali wa Watanzania, akimtakia mambo mema katika uamuzi unaotarajiwa kutolewa kesho.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments