Aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Geoffrey Mmari, amefariki dunia Oktoba 11, 2026, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu.
Kifo cha Profesa Mmari kimetokea takribani wiki tatu baada ya UDSM kumpoteza aliyekuwa makamu mkuu wake mstaafu, Balozi Nicholas Kuhanga, ambaye pia aliwahi kuwa Waziri wa Elimu nchini.
Katika maisha yake ya utumishi wa elimu ya juu, Profesa Mmari aliwahi kushika nafasi ya makamu mkuu katika vyuo vikuu mbalimbali, vikiwamo Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) na Chuo Kikuu cha Tumaini (TUDARCo).
Msiba wa marehemu uko nyumbani kwake, Masaki, Mtaa wa Mzinga Way, jijini Dar es Salaam.




