Monday, April 20, 2026
spot_img
HomeHabariNanauka aapa vijana kufaidika na fursa zilizopo nchini

Nanauka aapa vijana kufaidika na fursa zilizopo nchini

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana Joel Nanauka amesisitiza kuwa Wizara hiyo itaendelea kuwaweka Vijana katikati ya shughuli za kila siku, kwa kuhakikisha Vijana wanapata nafasi bila kubaguliwa, kuwashirikisha wa Mjini na Vijijini, wenye elimu na wasio na elimu na wa kutoka Vyama vyote vya siasa ili wote wanufaike na kufaidika na fursa za kiuchumi na kijamii.

‎”Hii ni Wizara ya Vijana wote na wote watanufaika kwa haki na usawa.” Amekaririwa akisema Nanauka leo Jumatatu Aprili 20, 2026 wakati akiwasilisha makadirio ya Bajeti ya Wizara yake kwa mwaka 2026/27, Bungeni Dodoma.

‎ Nanauka amebainisha kuwa wakati maeneo mengine wanatafsiri Vijana kama tatizo, serikali ya awamu ya sita kupitia Wizara ya maendeleo ya Vijana inawaona vijana kama mtaji mkubwa wa maendeleo ya nchi na zaidi katika kufanikisha utekelezaji wa Dira 2050, akibainisha kuwa maendeleo ya nchi yanategemea ubunifu wa vijana, mawazo na nguvu zao.

‎Nanauka amesema ni maono pia ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwafanya Vijana wa Kitanzania kutokuwa watazamaji bali washiriki na wamiliki wa uchumi wa Taifa lao kwa kupewa nafasi muhimu kwenye kuweka mipango, kushiriki kuweka vipaumbele na kuwa sehemu muhimu ya utekelezaji wa mipango ya serikali.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments