HomeElimuWanafunzi Goba Matosa wapokea msaada madawati, tangi la maji

Wanafunzi Goba Matosa wapokea msaada madawati, tangi la maji

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Goba Matosa iliyopo Wilaya ya Ubungo mkoani Dar es Salaam wamepokea msaada wa madawati 23 pamoja na tangi la kuhifadhia maji.

Msaada huo umetolewa na Fasthub Solutions ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa programu ya uwajibikaji kwa jamii.

Akizungumza wakati wa kutoa msaada huo, Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Taasisi hiyo, Christine Abulista amesema: “Tunaamini kuwa kuwekeza katika elimu ni kuwekeza katika mustakabali wa Tanzania. Kila mtoto anastahili kujifunza katika mazingira bora na salama”

Akipokea msaada huo, Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Matemanga amesema msaada huo utasaidia kupunguza changamoto ya uhaba wa madawati, huku tangi likiboresha upatikanaji wa maji kwa wanafunzi na walimu.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments