HomeHabariAjali ya mtumbwi Kilimanjaro yaua watano wa familia moja

Ajali ya mtumbwi Kilimanjaro yaua watano wa familia moja

Majonzi yamegubika Kijiji cha Chemchem, Kata ya Arusha Chini, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, baada ya watu watano wa familia moja kufariki dunia kufuatia ajali ya mtumbwi katika Bwawa la Nyumba ya Mungu.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kilimanjaro, Jeremia Mkomagi, amesema ajali hiyo ilitokea Julai 23, 2026 wakati waumini wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Chemchem walipokuwa wakielekea Kitongoji cha Mikocheni ‘B’ (Mikocheni Ndogo) kuhudhuria kongamano la Idara ya Wanawake.

Kwa mujibu wa Mkomagi, waliofariki ni wanawake wawili ambao ni dada wa familia moja pamoja na watoto watatu wa mmoja wao, wakiwemo wasichana wawili na mvulana mmoja.

Amesema mtoto mmoja wa familia hiyo pamoja na abiria wengine sita walinusurika ajali hiyo na baadhi yao walikimbizwa Hospitali ya TPC kwa matibabu baada ya kuokolewa.

“Tumefanikiwa kuopoa miili mitano kutoka majini na kuikabidhi Jeshi la Polisi kwa ajili ya taratibu nyingine. Uchunguzi unaendelea kubaini chanzo halisi cha ajali pamoja na kuthibitisha idadi kamili ya manusura na majeruhi,” amesema Mkomagi.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments