Kwa mujibu wa taarifa za awali kutoka Jeshi la Polisi, lori lililokuwa limebeba mchanga liligongana na lori lililokuwa likisafirisha kemikali aina ya sulphur, na kusababisha lori la mchanga kuteketea kwa moto.
Mwili wa mtu mmoja umetolewa kutoka kwenye lori lililoungua ukiwa umeharibika vibaya kutokana na moto.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Andrew Kantimbo amesema uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha ajali hiyo pamoja na kutambua idadi kamili ya walioathirika.
Taarifa zaidi zinatarajiwa kutolewa na Jeshi la Polisi baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa awali.












