Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids, anatarajiwa kutangazwa kuwa Kocha Mkuu mpya wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, imefahamika.
Fadlu anarejea nchini baada ya kutimuliwa na AS FAR Rabat ya Morocco kufuatia kutoipa matokeo mazuri katika Ligi Kuu ya nchi hiyo.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana jijini, Dar es Salaam jana zinasema kocha huyo ameshafikia makubaliano na Yanga kwa ajili ya kurithi mikoba iliyoachwa na Manqoba Mngqithi, raia wa Afrika Kusini.
Hata hivyo, Fadlu akiwa na Simba alishindwa kuwafunga Yanga katika mechi zote walizokutana.




