Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Samia Suluhu Hassan amesema Serikali yake katika miaka mitano ijayo, itakamilisha utekelezaji wa mradi wa Barabara ya Bagamoyo-Saadani-Pangani-Tanga.
Dk Samia ameyasema hayo leo, Jumatatu Septemba 29, 2025 alipozungumza na wananchi wa Pangani wakati wa mkutano wake wa kampeni za urais, uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi.
Amesema utekelezwaji wa mradi huo, utatengeneza muunganiko kati ya maeneo hayo na kusaidia kupunguza gharama za usafiri na kufungua milango ya uchumi.




