Monday, May 4, 2026
spot_img
HomeAfyaMchengerwa asisitiza huduma zenye staha

Mchengerwa asisitiza huduma zenye staha

Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa, amewataka watendaji, madaktari na wauguzi kutoa huduma kwa haki na kutumia lugha ya staha kwa wagonjwa na wananchi.

Akizungumza Mei 3, 2026 jijini Mwanza wakati akifungua Mkutano wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Wizara ya Afya, amesema serikali inaendelea kuboresha miundombinu na vifaa vya kisasa, lakini huduma bora haiwezi kukamilika bila utu na mawasiliano mazuri.

Amesisitiza kuwa wizara haitavumilia vitendo vya upendeleo, rushwa, lugha chafu na unyanyasaji kwa wagonjwa, akibainisha kuwa kauli nzuri inaweza kuwa sehemu ya tiba kwa mgonjwa.

Aidha, amesema wizara imekamilisha rasimu ya mwongozo wa motisha kwa watumishi ili kuongeza ari ya kazi, hususan kwa wanaofanya kazi katika mazingira magumu.

Kwa upande wake, Afisa Tawala Mkuu wa Wizara hiyo, Vivian Boniface, amesema watayafanyia kazi maelekezo hayo, huku Mwenyekiti wa Baraza hilo, Seif Shikalaghe, akisisitiza umuhimu wa kuwatambua na kuwathamini watumishi wa afya.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments