Tuesday, April 28, 2026
spot_img
HomeElimuTusitumie AI kutoa maoni ya ripoti ya tume, tuoneshe methodolojia zilizotumika

Tusitumie AI kutoa maoni ya ripoti ya tume, tuoneshe methodolojia zilizotumika

Baada ya Tume ya Rais ya Kuchunguza matukio ya wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2025 kutoa ripoti yake, kumekuwepo na maoni kutoka kwa watu mbalimbali ambayo kwa sehemu yanayotofautiana na maoni na mapendekezo ya Tume, kama ilivyoelezwa na mjumbe wa tume Jaji Mkuu mstaafu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma.

Akizunguza na wanahabari jijini Dar ea Salaam leo Aprili 28, 2027 Prof. Juma amesema maoni ya Tume yanatokana na mbinu (methodolojia) ya kisayansi na ushahidi ulio kusanywa, na hivyo ni muhimu kwa watu wengine wanaotoa maoni mbadala kuonyesha pia mbinu walizotumia kufikia hitimisho zao.

“Maoni yetu yanatokana na methodolojia na pengine ni vizuri wale watakaokuwa wanatoa maoni watasaidia sana jamii kama na wao watakuwa wanaonyesha methodolojia waliyotumia hadi kufikia yale maandiko, tusije kutumia methodolojia ya akili unde (AI), inakuandikia unafanya marekebisho kidogo unasema haya ni maoni yako,” amesema Prof. Juma.

Aidha amesisitiza kuwa maoni ya Tume yana uzito tofauti kutokana na msingi wake wa ushahidi, ambapo kila taarifa iliyotolewa ina uhalisia wa vyanzo vilivyokusanya ushahidi huo.

Awali, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Othman Chande, akielezea methodolojia zilizotumika kukusanya taarifa amesema Tume ilitumia mbinu mbalimbali zikiwamo ushahidi wa viapo kutoka kwa raia 953 na maafisa polisi 26, dodoso 4,891 zilizojazwa ikiwamo zile za mtandaoni, pamoja na mikutano ya makundi maalum 201 ya ana kwa ana iliyohudhuriwa na watu 3,565.

Ameongeza kuwa sehemu kubwa ya ushahidi uliokusanywa umetoka kwa waathirika wa matukio hayo kuliko maafisa wa polisi.

Aidha, Tume ilikutana ana kwa ana watu 6,205 ndani ya siku 153 katika mikoa 11 na wilaya 21 walizotembelea kukusanya taarifa hii ikionesha taarifa zilikusanywa kwa upana na urefu wa nchi yetu.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments