Wednesday, May 6, 2026
spot_img
HomeHabariBei Petroli yapanda tena Dar

Bei Petroli yapanda tena Dar

EWURA imetangaza ongezeko la bei ya mafuta ambapo lita moja ya petroli imepanda kwa Sh295 hadi kufikia Sh4,115 katika Dar es Salaam.

Bei hizo zimeanza kutumika Mei 5, 2026, huku EWURA ikieleza kuwa ongezeko hilo limetokana na kupanda kwa gharama za usafirishaji pamoja na athari za mvutano wa kimataifa kati ya Marekani, Israel na Iran.

Aidha, mamlaka hiyo imeeleza kuwa Serikali imeendelea kuchukua hatua za kupunguza athari kwa wananchi, ikiwemo kutoa ruzuku ya takribani Sh259 kwa kila lita ya dizeli ili kusaidia sekta ya usafiri.

Katika mabadiliko ya awali ya mwezi Aprili, bei ya petroli ilipanda kwa zaidi ya Sh900 kwa lita, hali inayoonesha mwenendo wa kuendelea kupanda kwa gharama za mafuta nchini.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments