Mkuu wa Kanda ya Kati wa Vodacom Tanzania Plc, Chiha Nchimbi (katikati), akifafanua kuhusu huduma ya Afya Mkopo kwa Naibu Waziri wa Afya, Dk. Florence Samizi, alipotembelea banda la huduma hiyo katika Kongamano la Wadau wa Sekta ya Afya Binafsi linaloendelea jijini Dodoma.
Kupitia ushirikiano kati ya Vodacom Tanzania Plc na PharmAccess Foundation kupitia Medical Credit Fund, huduma ya Afya Mkopo inalenga kuwawezesha watoa huduma binafsi wa sekta ya afya kupata mikopo nafuu na kwa urahisi.
Kwa kutumia mfumo wa LIPA NAMBA, watoa huduma hupata mikopo kwa haraka na masharti rafiki, hatua inayowawezesha kupanua huduma, kuboresha miundombinu na kukuza biashara zao.
Kushoto ni Dk. Heri Marwa, Mkurugenzi wa PharmAccess Foundation, na kulia ni Maula Mafuru, Meneja Mauzo wa M-Pesa Kanda ya Kati.








