Friday, November 7, 2025
spot_img
HomeMichezoMbeya City kurudi Ligi Kuu leo

Mbeya City kurudi Ligi Kuu leo

Baada ya kukosekana kwa misimu miwili, Mbeya City leo inarejea Ligi Kuu kwa mchezo wa kwanza dhidi ya Fountain Gate kwenye Uwanja wa Tanzanite, Manyara saa 8:00 mchana.

Timu hiyo ilishuka daraja msimu wa 2022/23 na sasa imerejea ikiongozwa na kocha Malale Hamsini, ambaye amesema wanahitaji alama tatu. Fountain Gate kupitia Ofisa Habari wao, Issa Mbuzi, wamesema wako tayari kwa changamoto hiyo.

Katika michezo mingine, Mashujaa FC watakabiliana na JKT Tanzania kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika saa 10:15 jioni, huku Namungo wakicheza na Pamba Jiji saa 1:00 usiku, Uwanja wa Majaliwa, Lindi.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments