HomeHabariNdoa ya Binti wa Ruto, Mtanzania kufungwa Mwanza Novemba 6

Ndoa ya Binti wa Ruto, Mtanzania kufungwa Mwanza Novemba 6

Charlene Ruto, binti wa Rais wa Kenya, William Ruto, anatarajiwa kufunga ndoa na mchumba wake, Isaya Yunge, mfanyabiashara kutoka Tanzania, katika hafla itakayofanyika jijini Mwanza.

Sherehe hiyo imepangwa kufanyika Novemba 6, 2026, katika fukwe za Hoteli ya Malaika Beach Resort jijini humo, huku maandalizi na shamrashamra za kuelekea tukio hilo zikianza kushika kasi.

Harusi hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka Tanzania na Kenya, akiwemo Rais wa Ruto, ambaye anatarajiwa kushiriki katika tukio hilo muhimu la kifamilia.

Ndoa hiyo inakuja baada ya wawili hao kufanya sherehe ya mahari na kuvishana pete ya uchumba Agosti 8, 2026, katika eneo la Kilgoris, Kaunti ya Narok nchini Kenya, iliyowakutanisha wana familia wa pande zote mbili katika hatua ya kuelekea kufunga ndoa.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments