HomeHabariSangu: PSSSF endeleeni kulipa mafao kwa wakati

Sangu: PSSSF endeleeni kulipa mafao kwa wakati

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, ameipongeza Mifuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa juhudi za kuboresha huduma na kuhakikisha wanachama na wastaafu wanapata mafao yao kwa wakati.

Sangu ametoa pongezi hizo Oktoba 13, 2026, alipotembelea banda la PSSSF katika maonesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Ndua, Manispaa ya Sumbawanga, mkoani Rukwa. Maonesho hayo yanafikia kilele leo, Oktoba 14, 2026.

“Hongereni, mnafanya kazi nzuri sana, endeleeni hivyo hivyo. Kabla ya kuja hapa, nilifungua semina ya wastaafu watarajiwa wa PSSSF na kuwaeleza kuwa chini ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dk. Samia Suluhu Hassan, Mfuko umeimarika na unaendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, ikiwemo kulipa mafao kwa wakati,” amesema Sangu.

Amehimiza PSSSF kuendeleza juhudi hizo ili wastaafu waendelee kupata huduma bora na kunufaika na mafao yao kwa wakati.

Katika maonesho hayo, PSSSF inatumia fursa hiyo kuwafikia wanachama na wananchi kwa ujumla, kutoa elimu kuhusu hifadhi ya jamii na kutoa huduma kwa wanachama, wakiwemo wastaafu.

Kupitia maonesho hayo, wananchi wanapata fursa ya kujifunza kuhusu umuhimu wa hifadhi ya jamii, maandalizi ya kustaafu na huduma mbalimbali zinazotolewa na Mfuko. Pia, wanaelezwa kuhusu maboresho yaliyofanyika katika mifumo ya utoaji huduma na mafao, yanayolenga kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wanachama.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments