Sunday, November 9, 2025
spot_img
HomeBiasharaVijana waaswa kujiwekea akiba kwa mustakabali bora

Vijana waaswa kujiwekea akiba kwa mustakabali bora

MbeyaKatibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Mhandisi Zena Ahmed Said, amewataka vijana nchini kujiwekea utamaduni wa kuweka akiba kupitia mifuko ya hifadhi ya jamii ili kuhakikisha usalama wa kifedha na ustawi wa maisha yao ya baadaye.

Amesema hatua hiyo itawawezesha vijana kupata huduma muhimu ikiwemo mikopo, matibabu, mafao ya uzeeni, pamoja na fursa nyingine za kiuchumi zinazotolewa na mifuko hiyo.

Mhandisi Zena alieleza hayo Oktoba 13, 2025, wakati akifunga Kongamano la Siku Mbili la Vijana, lililofanyika katika Ukumbi wa City Park Garden, Mbeya.

“Kijana mwenye utamaduni wa kuweka akiba ni kijana mwenye dira ya mafanikio, anayejali kesho yake na anayechangia katika maendeleo ya taifa,” alisema Mhandisi Zena.

Aidha, alisisitiza umuhimu wa vijana kuwekeza katika mustakabali wao kwa kupanga matumizi yao na kujiunga na mifumo rasmi ya hifadhi ya jamii.

Pia, amewahimiza vijana kudumisha uzalendo, kuepuka vitendo vya uvunjifu wa amani na kujiepusha na makundi yanayopandikiza chuki au misimamo mikali.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments