Thursday, March 5, 2026
spot_img
HomeHabariNaibu Waziri Kisuo ataka PSSSF kuendelea na miradi yenye tija

Naibu Waziri Kisuo ataka PSSSF kuendelea na miradi yenye tija

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano Rahma Kisuo amesema kuwa serikali itaendelea kuuunga mkono miradi yenye tija inayozalisha ajira kwa vijana wa kitanzania, itakayolinda na kuimarisha hifadhi ya jamii, na inayoongeza ushindani kwa maendeleo ya Taifa.

Aidha Kisuo ameupongeza Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa uwekezaji wa miradi yenye tija kwa maendeleo ya Taifa ikiwemo Mradi wa Mount Kilimanjaro International Conventional Centre (MK – ICC) na mradi wa nyumba za makazi wa Oloirien, ambapo amewaasa kuhakikisha miradi wanayowekeza izalishe ajira za vijana kwa wingi na hatimae kukuza maendeleo ya nchi kwa ujumla
Ametoa pongezi hizo leo Januari 6, 2026 JIjini Arusha wakati wa ziara yake ya kikazi inayolenga kukagua miradi hiyo ambapo mradi MK – ICC ni mradi unaotekelezwa kwa miezi 18 na unaogharimu Bilioni 429.38 ukijumuisha gharama za ujenzi wa ukumbi mkubwa wa mikutano unaoweza kuhudumia watu 5,000 kwa wakati mmoja, kumbi ndogo za mikutano zenye uwezo wa kuhudumia watu kuanzia 50 mpaka 500.

Sambamba na hayo yote Naibu Waziri Kisuo ametoa wito kwa PSSSF kuutangaza mradi huo kwa kiasi kikubwa pale utakapokamilika ili kuvutia wateja wa ndani nan je ya nchi na hivyo kuwa na uhakika wa mapato kupitia mradi huu.

“Mradi mkubwa kama huu unaoajiri vijana wengi pia unahitaji matangazo makubwa, tutangaze na tutafute wateja wa ndani nan je ya nchi zikiwemo taasisi za kimataifa na kikanda waje kutumia mradi huu,” amesema Naibu Waziri na kusisitiza kwa PSSSF kuendelea kuwekeza kwenye miradi yenye tija na kulinda fedha za wananchama wa PSSSF lakini pia miradi isimamiwe kwa umakini.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Fortunatus Magambo, alimhakikishia Naibu Waziri kuwa Mfuko umejipanga kusimamia miradi hiyo kwa uadilifu wa hali ya juu ili kufikia malengo ya kurejesha mtaji na faida iliyokusudiwa.

Alibainisha kuwa mradi wa MK-ICC umezingatia vigezo vyote vya kisasa na unatarajiwa kuwa kichocheo kikubwa cha uchumi na utalii nchini, huku ukitoa kipaumbele kwa wataalamu na vijana wa Kitanzania katika hatua zote za utekelezaji hadi uendeshaji wake.

Aidha, Mkurungenzi Mkuu Magambo aliongeza kuwa Mfuko utafanyia kazi maelekezo ya Serikali kuhusu utafutaji wa masoko ya kimataifa ili kuhakikisha kituo hicho kinakuwa na shughuli mwaka mzima.

“Ushirikiano kati ya PSSSF na AICC kupitia kampuni ya uendeshaji (SPV) utahakikisha kuwa mradi huu unajiendesha kwa ufanisi, unaleta tija kwa wanachama, na unachangia kwa kiasi kikubwa kuchochea ajira za vijana na pato la Taifa kupitia sekta ya Utalii ambayo ni msingi wa ukanda huu wa kaskazini,” amesema Magambo.

Kesho (Jumatano, Januari 7, 2026) Naibu Waziri Kisuo anaendelea na ziara yake katika mkoa wa Kilimanjaro ambapo atatembelea kiwanda cha biadhaa za ngozi kinachomilikiwa kwa ubia kati ya PSSSF na Jeshi la Magereza.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments