HomeMichezoAhmed Ally awataka Simba kumsahau Mwalimu, kuelekeza nguvu Ngao ya Jamii

Ahmed Ally awataka Simba kumsahau Mwalimu, kuelekeza nguvu Ngao ya Jamii

Baada ya Klabu ya Yanga kumtangaza Selemani Mwalimu katika kikosi chao, Meneja wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally ameandika ujumbe mzito ulioambatana na picha ya kikosi cha Simba, akiwatia moyo mashabiki na kuwataka waendelee kuipigania kesho ambayo ni siku ya Mchezo wao muhimu wa Ngao ya Jamii dhidi ya watani wao wa jadi Yanga.

“Wengi tumeingia kwenye taharuki baada ya kuona aliyekua mshambuliaji wetu kutambulishwa klabu nyingine. Kwanza niwape pole Wana Simba kwa taharuki hii. Sipo hapa kujielezea nini kimetokea, Kitu muhimu zaidi kwa sasa tuwekeze nguvu kwenye mchezo wetu wa kesho wa Ngao ya Jamii”

“Hakuna tunachokihitaji zaidi ya ushindi, kwa misimu miwili tumeikosa Ngao ya Jamii, Huu ndio wakati sahihi wa kuchukua Taji hili Insha Allah

Akili yetu, fikra zetu, mawazo yetu na nguvu zetu tuzielekeze Amaan Stadium, Safati hii tunatakiwa kuufungua msimu kwa Ubingwa wa Ngao

Tumerithishwa kuipenda Simba yetu hivyo tuendelee kuipigania kesho tupate furaha ya wote”,ameandika Ahmed Ally

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments