Saturday, March 21, 2026
spot_img
HomeHabariDC Nyamwese atoa siku 21 mageti ya Soko la Chogo-Handeni yarekebishwe

DC Nyamwese atoa siku 21 mageti ya Soko la Chogo-Handeni yarekebishwe

Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Salum Nyamwese, ametoa wiki tatu kwa Halmashauri ya Mji Handeni kufanya maboresho mbalimbali katika Soko la Chogo, ikiwamo kurekebisha mageti ya kuingilia sokoni, ili kudhibiti tatizo la wizi wa bidhaa za wafanyabiashara.

Nyamwese ametoa agizo hilo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika soko hilo na kusikiliza changamoto zinazowakabili wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao katika eneo hilo.

Amesema dhamira ya Serikali ni kuhakikisha wafanyabiashara wanafanya shughuli zao katika mazingira safi, salama na rafiki, ili waweze kutoa huduma bora kwa wananchi bila hofu ya usalama wa mali zao.

Aidha, katika ziara hiyo, Nyamwese ameelekeza Halmashauri ya Mji Handeni kufanya marekebisho ya haraka ya mageti ya kuingilia sokoni hapo ili kudhibiti wizi wa mara kwa mara wa bidhaa za wafanyabiashara, jambo ambalo limekuwa likisababisha hasara kwao.

“Hali ya usafi katika lile dampo hairidhishi. Mrundikano wa taka uliopo unahatarisha afya za wananchi na wafanyabiashara. Naiagiza Halmashauri kwa kushirikiana na viongozi wa soko kuangalia namna bora ya kuhakikisha taka zinaondolewa kwa haraka pindi zinapokusanywa,” ameagiza.

Naye, Afisa Biashara wa Halmashauri wa Mji Handeni, Paul Lusinde, ameahidi kufanyia kazi maagizo ya Mkuu huyo.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments