Friday, February 20, 2026
spot_img
HomeBiasharaSangu aipongeza CRDB kwa Ughaibu Loan

Sangu aipongeza CRDB kwa Ughaibu Loan

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mheshimiwa Deus Sangu ameipongeza Benki ya CRDB kwa ubunifu wake wa kuwawezesha Watanzania wanaopata ajira nje ya nchi kukidhi mahitaji ya kifedha kupitia Ughaibu Loan.

Waziri Sangu ametoa sifa hizo kwenye mkutano wa wizara yake na Chama cha Mawakala Binafsi 148 wa Ajira za Nje yaani Tanzania Recruitment Agency Association (TRAA) pamona na wadau wengine kuzingatia mwongozo wa uratibu wa ajira za nje ya nchi ili kuwanufaisha Watanzania wengi zaidi.

“Zamani hakukuwa na utaratibu rasmi wa Mtanzania anayepata ajira ya nje. Tumeanzisha mifumo ya kisheria na ya kitaasisi inayosimamia ajira za ndani na nje ya nchi ili kuondoa vikwazo vilivyokuwepo zamani,” amesema Waziri Sangu na kuongeza:

“Nawashukuru sana Benki ya CRDB inayosaidia kuwalipa vijana wote wanaopata kazi nje ya nchi kwani wameanzisha ughaibuni loans ambayo inampa kijana mkopo wa mpaka shilingi milioni 20 kumwezesha kulipia pasipoti, visa na kukidhi mahitaji mengine muhimu fedha atakazoilipa pindi akifika aendako na kuanza kupokea mshahara wake.”

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB, Stephen Adili amesema dhamira ya Benki ya CRDB ni kuboresh amaisha ya Watanzania kwa kuleta huduma zinazokidhi mahitaji ya mteja.

“Sisi ni benki inayomsikiliza mteja. Tunawaahidi wateja wetu kuwapa huduma bora wakati wote na tupo tayari kuendelea kubuni bidhaa rafiki zaidi ili wafanikishe malengo yao,” amesema Adili.

Takwimu za serikali zinaonyesha kwa kipindi cha kuanzia Januari 2026 hadi sasa Watanzania 2,002 wamepata ajira nje ya nchi.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments