Thursday, March 26, 2026
spot_img
HomeHabariWaziri Mkuu awaomba watanzania kumuombea Hayati Lukuvi

Waziri Mkuu awaomba watanzania kumuombea Hayati Lukuvi

Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba, amewaomba Watanzania kuendelea kumuombea aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, marehemu William Lukuvi, aliyefariki dunia Machi 25, 2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.

Akizungumza kwa niaba ya Serikali nyumbani kwa marehemu eneo la Area D, Dodoma, Machi 26, 2026, Waziri Mkuu alisema kifo hicho ni pigo kubwa na jambo gumu kulielewa.

“Kwa niaba ya Serikali, natoa pole kwa familia, ndugu na jamaa. Jambo hili ni zito na hatukulitarajia, kwani Mheshimiwa Waziri alikuwa bado anatekeleza majukumu yake,” alisema.

Amesisitiza umuhimu wa kuendelea kumuombea marehemu pamoja na kuifariji familia katika kipindi hiki kigumu, akieleza kuwa Mwenyezi Mungu ndiye mfariji mkuu.

Aidha, Dkt. Nchemba ameihakikishia familia kuwa Serikali itaendelea kuwa pamoja nayo katika kipindi chote cha maombolezo.

Viongozi wengine waliohudhuria msiba huo ni pamoja na Naibu Spika Daniel Siro, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Hamad Masauni, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) Ridhiwani Kikwete, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Toba Nguvila.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments