Tuesday, May 5, 2026
spot_img
HomeMichezoRais Samia amkaribisha Drogba kuwa Balozi wa AFCON 2027

Rais Samia amkaribisha Drogba kuwa Balozi wa AFCON 2027

Rais Samia Suluhu Hassan amemkaribisha mshambuliaji wa zamani wa Ivory Coast, Didier Drogba, kuwa balozi maalum wa Tanzania kuelekea fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2027.

Rais Samia ametoa mwaliko huo leo Jumanne, Mei 5, 2026, Ikulu Chamwino jijini Dodoma wakati akizungumza naye, ikiwa ni siku chache baada ya Drogba kuwasili nchini na kushiriki Bunge la Bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo jana Mei 4, 2026.

Aidha, Rais Samia ameielekeza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kushirikiana na nyota huyo wa zamani wa Chelsea F.C. katika kubadilishana uzoefu wa usimamizi na uendelezaji wa akademia za michezo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha sekta ya michezo nchini.

Kwa upande wake, Drogba ameshukuru kwa mwaliko huo na kuonesha utayari wa kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuendeleza michezo.

Drogba anachukuliwa kuwa mmoja wa wanasoka waliopata mafanikio makubwa duniani na pia anasifiwa kwa mchango wake katika juhudi za amani nchini Ivory Coast mwaka 2005, alipotumia ushawishi wake kusaidia kukomesha mgogoro wa muda mrefu wa kivita.


RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments