Saturday, April 25, 2026
spot_img
HomeMichezoDabi ya Kariakoo kuhamishiwa Isamuhyo Mei 3

Dabi ya Kariakoo kuhamishiwa Isamuhyo Mei 3

Mchezo wa pili wa Dabi ya Kariakoo katika Ligi Kuu Bara msimu wa 2025/26 kati ya wenyeji Simba SC na mahasimu wao Young Africans SC utafanyika Mei 3, 2026 saa 12:00 jioni katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo.
‎
‎Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Aprili 24, 2026 na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, mchezo huo uliokuwa upigwe katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Stadium umehamishwa kutokana na dimba hilo kuwa kwenye matengenezo.
‎
‎TPLB imeeleza kuwa klabu zote mbili pamoja na wadau wa Ligi Kuu ya NBC wamepatiwa taarifa kuhusu mabadiliko hayo, huku maandalizi ya mchezo huo yakianza mara moja.
‎
‎Dabi hiyo yenye ushindani mkubwa inatarajiwa kufanyika katika viwango vya juu, ikiakisi hadhi ya Ligi Kuu ya Tanzania ambayo inaendelea kushika nafasi ya sita kwa ubora barani Afrika.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments