HomeHabariMhubiri Mackenzie afungwa miaka 200 kwa mauaji Shakahola

Mhubiri Mackenzie afungwa miaka 200 kwa mauaji Shakahola

Mhubiri Paul Mackenzie amehukumiwa kifungo cha miaka 200 jela baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika na mauaji ya wafuasi 191 wa kanisa lake la Good News International.

Hukumu hiyo imetolewa na Jaji Diana Kavedza, huku washtakiwa wengine katika kesi hiyo wakihukumiwa vifungo vya kati ya miaka 10 na 160 jela.

Miongoni mwa waliouawa ni watoto 190 na mtu mzima mmoja. Mauaji hayo yanadaiwa kufanyika kati ya mwaka 2021 na 2023.

Taarifa ya ziada iliyothibitishwa: Kwa mujibu wa Reuters, kifungo cha miaka 200 kinajumuisha miaka 100 kwa mauaji yaliyotokana na njaa ya kulazimishwa na miaka 100 kwa mauaji ya moja kwa moja.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments