Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) imetumia Maonesho ya Tisa ya Kimataifa ya Uagizaji wa Bidhaa ya China (CIIE), jijini Shanghai, kutangaza mazao ya Tanzania na kuvutia wanunuzi wa kimataifa kupitia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala.
Katika maonesho hayo yanayofanyika Novemba 5–10, 2026, WRRB imeeleza namna mfumo huo unavyowezesha kuhifadhi mazao katika maghala yenye leseni, kudhibiti ubora na kuyauza kwa uwazi.
Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Omar Said Shabaan, amepongeza ushiriki wa Tanzania, akisema maonesho hayo yanatoa fursa kwa taasisi kutangaza huduma na bidhaa za nchini kwa wanunuzi wa kimataifa.
Naye mwakilishi wa kampuni ya Chengdu Jintao Yunhui International Trade Co., Ltd. ameonesha kuvutiwa na ufuta mweupe wa Tanzania, unaouzwa kupitia mfumo huo.






