HomeHabariTrump adai hapokei mshahara wa urais wa Marekani, yeye ni tajiri

Trump adai hapokei mshahara wa urais wa Marekani, yeye ni tajiri

Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema hafuatilii kiwango cha utajiri wake kwa kuwa ana fedha nyingi, akibainisha kuwa pia hapokei mshahara wa urais.

Trump ameyasema hayo katika mahojiano maalumu na kipindi cha 60 Minutes kinachorushwa na kituo cha televisheni cha CBS, alipoulizwa kuhusu taarifa za jarida la Forbes zinazoonyesha kuwa utajiri wake umeongezeka kwa takribani dola bilioni tatu za Marekani.

Akijibu swali hilo, Trump amesema hana muda wa kufuatilia kiwango cha utajiri wake, ingawa anakiri kuwa huenda umeongezeka.

“Sina muda wa kufuatilia nina utajiri wa kiasi gani. Sijali, nina pesa nyingi sana na nahisi utajiri wangu umeongezeka, lakini sijui. Kikubwa nina mwanangu ambaye anasimamia na kutunza fedha zangu, na wala sizungumzi naye kuhusu fedha hizo,” amesema.

Ameongeza kuwa alikuwa na utajiri mkubwa hata kabla ya kuingia madarakani na kwamba hapokei mshahara wake kama Rais.

“Nina pesa nyingi na nilikuwa na pesa nyingi hata kabla ya kuwa Rais, sichukui hata mshahara,” amesema Trump.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments