Singida Black Stars wameanza safari kuelekea Rwanda kwa mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Rayon Sports Jumamosi hii.
Kocha Mkuu, Miguel Gamond, amesema baada ya kutwaa ubingwa wa Kagame, nguvu sasa zimeelekezwa kwenye michuano ya kimataifa.
Gamond amesema wachezaji wako na morali kubwa na wamefanyia kazi mapungufu yaliyoonekana kwenye Kagame Cup.
Ameomba watanzania kuwaombea dua ili wapate ushindi kwenye mchezo huo mgumu unaotarajiwa Kigali.








