MIXX, kampuni inayoongoza katika huduma za kifedha kwa njia ya simu, limeendelea na uzinduzi wa kampeni yake ya “Kila Hatua Mixx” jijini Mbeya, Septemba 16, 2025.
Lengo likiwa , kuongeza ujumuishwaji wa kifedha na kuimarisha uchumi wa kidijitali katika Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.
Kanda hiyo ni kiungo muhimu cha uchumi wa Tanzania, ikiwa ni ghala kuu la chakula, lango la biashara kuelekea nchi za Kusini mwa Afrika, na kitovu cha shughuli za kilimo, usafirishaji na ujasiriamali unaokua kwa kasi.
Akizungumza na waandishi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni hiyo Mkurugenzi wa Yas Kanda ya Nyanda za juu Kusini, Abbas Abdurahamani amesema Kanda hiyo ni injini ya maendeleo ya taifa, ambayo inaunganisha wakulima, wafanyabiashara, na masoko ya kikanda.
“Uzinduzi wa ‘Kila Hatua Mixx’ hapa Mbeya ni ishara ya kuendeleza ubunifu wetu kwa kuwaletea watanzania suluhisho za kifedha zinazojibu changamoto za wakazi wa kanda hii.
“Tutaendelea kushirikiana kwa karibu na washirika wetu wote ili kuendeleza mageuzi ya kidijitali na ukuaji wa uchumi shirikishi,” amesema Abbas


Amesema, Takwimu za Mixx zinaonyesha matokeo makubwa ya kitaifa:Watumiaji milioni 20+ hufanya miamala kila mwezi yenye thamani ya takribani TSh trilioni 6.Agenzi 200,000+ wameunda ajira zisizo za moja kwa moja kwa maelfu ya vijana.
Aidha, amesema Wafanyabiashara 500,000+ hupokea malipo kidijitali kupitia mifumo ya Mixx.Taasisi na mashirika 3,000+ hutumia Mixx kwa makusanyo na malipo makubwa.
Pia, Wateja milioni 6+ wamepata mikopo yenye thamani ya zaidi ya TSh trilioni 1, huku zaidi ya TSh bilioni 600 zikiwa zimewekwa kama akiba.
Vilevile amesema, bidhaa na huduma zinazojumuishwa katika kampeni ni pamoja na:Bustisha – Mikopo midogo ya muda mfupi kuhakikisha miamala haikatiki.Nivusheplus – Mikopo ya papo kwa hapo kwa dharura au mtaji wa biashara.
Amesema, Kibubu – Zana ya kidijitali ya kuweka akiba kwa malengo ya kifedha ya muda mrefu. Lipa kwa Simu – Malipo salama kwa wafanyabiashara wadogo na wakubwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Biashara – Mixx, James Sumari amesema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ni soko lenye nguvu na uthubutu – iwe ni kwa wakulima au wajasiriamali.
“Huduma zetu zinalenga kuziwezesha jamii hizi kuendeleza biashara, kuongeza mitaji, na kushiriki kikamilifu katika uchumi wa kidijitali.
“Mixx si tu mtoa huduma za kifedha bali ni mshirika wa karibu wa kila mtanzania katika kuhakikisha jamii nzima inastawi kiuchumi,” amesema.
Hata hivyo amesema, Kwa kuwekeza kwenye huduma ya haraka salama na rahisi kutumia, Mixx inalenga kuhakikisha wakulima, wafanyabiashara wadogo na kati, na Taasisi mbalimbali katika Kanda hiyo inayojumuisha mkoa wa Mbeya, Njombe, Ruvuma, Rukwa na Katavi wanapata fursa sawa za kifedha na kidijitali kama wenzao katika miji mikuu.
Uzinduzi huo, ni dhamira ya Mixx kugusa kila ngazi ya uchumi, kuanzia biashara ndogo ndogo hadi uwekezaji wa kiwango cha juu – ili kuharakisha kasi ya uchumi wa kidijitali wa Tanzania.





