Katika mkutano huo uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi wa Kagera, Dk Samia Suluhu Hassan amesema wakati wa uendeshaji wa mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Chongoleani Tanga utatoa fursa nyingine.
Dk Samia amewaahidi wananchi Kagera akipata ridhaa ndani ya miaka mitano ijayo atakamilisha ujenzi wa barabara ya Rusaunga- Rusumo yenye thamani ya Sh 153.5 bilioni.
“Ujenzi wa barabara zingine ni Murugarama-Rulenge hadi Nyakaula kilomita 85 na kujenga kwa lami barabara ya Kajai-Bwanjai hadi Buyangu, sambamba na barabara za lami za Mutukula mjini zipo kwenye ilani,” amesema.
Mbali na hilo, Dk Samia amesema maboresho makubwa ya bandari Kemondo yameenza kwa kuongeza urefu wa gati na kuongeza wigo wa lango la meli ili ziweze kupakia na kushusha bidhaa.
“Lengo ni kuwezesha meli kubwa za mizigo na abiria kutia nanga katika bandari ya Kemondo. Mamlaka ya Bandari Tanzania ina miliki eneo la ekari 100 kwa ajili ya kuweka miundombinu muhimu ikiwemo mifumo ya maghala,” ameeleza.
Kuhusu bandari ya Bukoba, Dk Samia amesema imefanyiwa marekebisho makubwa iliyohusisha ukarabati wa magati matatu, uchimbaji ili kuongeza kina, ujenzi wa jengi jipya la abiria takribani 700.
“Maboreshio haya bandari yamelenga kuhudumia meli kubwa za kisasa ikiwemo ya New Mv Mwanza,”
“Kwa upande wa usafiri wa anga, kwa kuzingatia ufinyu wa kiwanja cha ndege cha Bukoba, ndani ya miaka mitano ijayo tunajipanga kujenga kiwanja kipya cha ndege cha kimataifa cha Mkoa wa Kagera.
Kuhusu mafuriko ya Mto, Kanoni Bukoba Mjini Dkt Samia amesema taratibu za ujenzi zimekamilika na wakati wowote utaanza ili kukabiliana na changamoto hizo.
Mbali na hilo, Dkt Samia amesema upembuzi yakinifu wa mradi umeme wa Kakono -Misenyi upembuzi yanikifu umekamilika, huku mradi wa Nsongezi-Kyerwa ukiwa katika hatua ya maandalizi ya awali ya ujenzi.
“Pia tutajenga vituo vya kupoza na kusambaza umeme ili kuwa na uhakika wa umeme muda wote,”
“Tunataka umeme wa kutosha kwa ajili ya kutekeleza mradi wa kongani za viwanda na matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Kwenye maji tupo, vizuri tunataka kila Mtanzania, awe karibu na maji safi na salama,” amesema Dk Samia.
Katika sekta ya uvuvi, Dk Samia amesema ndani ya miaka mitano ijayo tutawajengea uwezo wavuvi kwa kuwapa mafunzo na nyenzo (mitaji, mikopo na vyombo vya kisasa) ili kufanya shughuli za kwa ufanisi.
Pia, Dk Samia amewakumbuka wamachinga akiwaahidi ujenzi wa soko kubwa Bukoba Mjini eneo la Kishenye ambapo Sh 10bilioni zimetengwa kwa ajili ya mchakato huo.




