Wednesday, May 6, 2026
spot_img
HomeHabariDkt Samia: Mkipata vyeo msivimbe

Dkt Samia: Mkipata vyeo msivimbe

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, amewaambia watendaji wa Serikali kuwa vyeo ni dhamana, akisema ni dhambi kubwa mtu kupata cheo kisha kuvimba mabega.

Ametoa rai hiyo leo Jumatano wakati akiwaapisha wateuliwe mbalimbali alioteua wiki iliyopita. Hafla hiyo imefanyika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Mkuu huyo wa nchi, amesisitiza kuwa cheo ni dhamana na dhambi kubwa ukapata cheo, ukavimbisha mabega, ukawa untouchable ‘usiyegusika’ we unanijua mi nani who are you?

Katika msisitizo wake, Dkt Samia amesema, “Narudia tena wewe nani? Wewe ni kiumbe kama wengine, ila Mungu ameamua kushika hapo.

“Amekupa hapo ili uwatumikie watu, kama ni sadaka yako ukiwa duniani,” amesema.

Kwa mujibu wa Rais Dkt Samia kama hutumikii vyema watu, Mungu anajua na ana adhabu zake na kwamba Serikali inapitia tu, lakini mambo yote ni Mungu.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments