Monday, March 9, 2026
spot_img
HomeHabariDk. Samia aombeleza waliokufa Oktoba 29, aunda Tume kuchunguza

Dk. Samia aombeleza waliokufa Oktoba 29, aunda Tume kuchunguza

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan amesema ameombeleza vifo vilivyotokea katika vurugu za Oktoba 29, huku akisema ameunda Tume itakayochunguza kadhia hiyo.

Dk. Samia ametoa kauli hiyo, leo Ijumaa Novemba 14,2025 wakati akihutubia Bunge jijini Dodoma, ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa Bunge la 13, ambapo pamoja na mambo mengine alitoa mwelekeo wa Serikali yake kwa miaka mitano ijayo.

Kabla ya kuhutubia, Dk. Samia aliwaomba wabunge na wageni waalikwa kusimama kwa dakika moja kuwaombea.

“Nianze na jambo la huzuni lilitokea hapa nchini, niwaombe waheshimiwa wabunge kusimama kwa dakika moja kuwaombea…Tumuombe mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu waliopoteza maisha kwenye vurugu zilizotokea Oktoba 29,” amesema.

“Nimehuzunishwa sana na tukio lile natoa pole kwa familia zote zilizopoteza familia zao. Kwa majeruhi tunawaombe wapone haraka, Serikali imechukua ya kuunda Tume kuchunguza yaliyotokea ili kujua kiini cha tatizo,”

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments