Sunday, November 9, 2025
spot_img
HomeBiasharaDkt Samia aahidi ujenzi Barabara Kibiti-Mtumba

Dkt Samia aahidi ujenzi Barabara Kibiti-Mtumba

Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Samia Suluhu Hassan amesema katika miaka mitano ijayo, Serikali yake itajenga Barabara ya Bungu-Nyamisati, Kibiti-Mtumba na Rufiji-Mbwela.

Dk Samia ametoa ahadi hiyo leo, Jumatatu Oktoba 20, 2025 alipozungumza na wananchi wa Kibiti mkoani Pwani, katika mkutano wake wa kampeni za urais.

Ameahidi kujenga Barabara ya Bungu-Nyamisati, Kibiti-Mtumba, Rufiji-Mbwela na kuboresha barabara za ndani zikiwemo kilomi 42 za maeneo korofi ili zitumike misimu yote.

Dk Samia amesema miradi ya maji 23 imekamilishwa wilayani humo na kuongeza upatikanaji wa huduma hiyo kutoka asilimia 47 hadi 74 na kwamba ataendelea kuboresha kuhakikisha wananchi wanapata maji zaidi Kibiti.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments