HomeElimuProf. Mkenda: Tushirikiane kulinda haki za watoto

Prof. Mkenda: Tushirikiane kulinda haki za watoto

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, ametoa wito kwa wazazi, walezi, viongozi wa dini, mashirika na wadau mbalimbali wa maendeleo kushirikiana na Serikali kuhakikisha kila mtoto anapata haki zake za msingi, ikiwemo elimu bora, huduma za afya, maji safi na mazingira salama ya kukua na kuendelea.

Prof. Mkenda amesema hayo Juni 16, 2026 jijini Dodoma wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika, akieleza kuwa siku hiyo ni ukumbusho kwa jamii kuhusu wajibu wa kulinda, kuheshimu na kuendeleza haki za watoto, sambamba na kumbukumbu ya watoto wa Soweto nchini Afrika Kusini waliopigania haki ya kupata elimu bora.

Amesema Serikali  inaendelea kuweka elimu kuwa kipaumbele kikuu kwa kuzingatia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na maelekezo ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan  kuhakikisha kila mtoto wa Kitanzania anapata elimu.

Kwa mujibu wa Prof. Mkenda, Serikali imeendelea kuimarisha usawa na ujumuishi katika elimu ili watoto wote, bila kujali hali zao, wapate fursa ya kujifunza na kutimiza ndoto zao.

“Hakuna mtoto atakayeachwa nyuma katika mfumo wa elimu. Hata mabinti waliopata ujauzito wanaruhusiwa na wanapaswa kurejea shuleni kuendelea na masomo yao,” amesema Prof. Mkenda.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha shule zinakuwa mazingira salama na rafiki kwa watoto ili kuwawezesha kujifunza kwa ufanisi na kufikia malengo yao kielimu.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments