HomeBiasharaMji wa Serikali Mtumba kuwa mfano wa matumizi ya nishati safi kupitia...

Mji wa Serikali Mtumba kuwa mfano wa matumizi ya nishati safi kupitia gesi asilia


‎DAR ES SALAAM– Serikali inaendelea na maandalizi ya kuufanya Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma, kuwa mfano wa matumizi ya nishati safi kupitia mradi wa usambazaji wa gesi asilia utakaohudumia taasisi za umma, biashara na makazi.

‎Hayo yameelezwa na Mjiolojia kutoka Wizara ya Nishati, Nuru Helambili, wakati akitoa elimu kwa wananchi wanaotembelea banda la wizara hiyo katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba).

‎Helambili amesema miundombinu ya mradi huo itaunganisha gesi asilia katika majengo ya wizara, ofisi za ubalozi, taasisi za Serikali, majengo ya biashara, hoteli, migahawa pamoja na makazi yaliyopo eneo la Mtumba

‎Amesema mradi huo unalenga kujenga kituo cha kupokelea gesi asilia (Gas Receiving Terminal), ambapo gesi itakuwa ikisafirishwa kwa magari maalumu kutoka Kituo Mama cha Gesi Asilia kwa Magari (CNG) kilichopo Mlimani City, Dar es Salaam.


‎Aidha, amesema mradi huo utahusisha ujenzi wa kituo cha kupunguza mgandamizo wa gesi, mtandao wa usambazaji wa gesi pamoja na kituo cha kujazia gesi asilia kwenye magari.

‎Helambili amesema katika mwaka wa fedha 2026/2027, Serikali itakamilisha tathmini ya athari kwa mazingira na jamii (ESIA) na kuanza taratibu za kumpata mkandarasi wa utekelezaji wa mradi huo.

‎Ameongeza kuwa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limetenga Sh bilioni 14.40 kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za awali za mradi huo, unaotarajiwa kuimarisha matumizi ya nishati safi na kuchochea maendeleo ya Mji wa Serikali Mtumba.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments