HomeAfyaTanzania, Marekani zasaini makubaliano ya Dola Bilioni 3.14 kuimarisha sekta ya afya

Tanzania, Marekani zasaini makubaliano ya Dola Bilioni 3.14 kuimarisha sekta ya afya

Serikali za Tanzania na Serikali ya Marekani zimesaini Hati ya Makubaliano (MoU) ya ushirikiano katika sekta ya afya ya miaka mitano itakayotekelezwa kuanzia mwaka 2026 hadi 2030, yenye thamani ya zaidi ya dola za Marekani bilioni 3.14 kupitia uwekezaji wa pamoja wa nchi hizo mbili. 

Makubaliano hayo yanajengwa juu ya mafanikio ya ushirikiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na Marekani katika sekta ya afya, yakilenga kuimarisha mifumo ya afya kwa kuboresha hospitali, maabara na uwezo wa wataalamu wa afya, ili kuboresha utoaji wa huduma, kuongeza uwezo wa Tanzania kujitegemea katika kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza na kuimarisha utayari wa nchi kuzuia na kukabiliana na milipuko ya magonjwa pamoja na dharura za afya siku zijazo.

Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini iliyofanyika Dar es Salaam Julai 1, 2026, Waziri wa Afya, Mohamed Omary Mchengerwa, amesema Marekani itachangia takribani dola bilioni 1.34 huku Tanzania ikiahidi kuchangia zaidi ya dola bilioni 1.8 katika kipindi hicho. 

Amesema makubaliano hayo yanaashiria hatua mpya ya ushirikiano unaojengwa katika misingi ya usawa, uwajibikaji na kujitegemea badala ya utegemezi wa muda mrefu.

“Makubaliano haya si mwendelezo wa utegemezi bali ni ramani ya kutuondoa kwenye utegemezi. Ifikapo mwaka 2030 Tanzania ndiyo itakayobeba sehemu kubwa ya gharama za mfumo wake wa afya,” amesema Waziri Mchengerwa.

Kupitia makubaliano hayo, Marekani itaelekeza msaada wake katika kutekeleza vipaumbele vya sekta ya afya vya Tanzania na kuiwezesha nchi kunufaika na utaalamu katika dawa, ubunifu wa afya na teknolojia za tiba, mapambano dhidi ya UKIMWI, malaria, polio na kifua kikuu na kuimarisha huduma za afya ya mama na mtoto.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments