HomeHabariPSSSF yakabidhi miradi ya maji shule mbili Dodoma

PSSSF yakabidhi miradi ya maji shule mbili Dodoma

Zaidi ya watu 1,000, wakiwemo wanafunzi na walimu, wanatarajiwa kunufaika na upatikanaji wa huduma ya maji kupitia miradi miwili ya visima iliyotekelezwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) katika shule mbili mkoani Dodoma.

Miradi hiyo yenye thamani ya Sh milioni 55 imekabidhiwa katika Shule ya Sekondari Kimaghai, iliyopo Mpwapwa, na Shule ya Msingi Uhuru, jijini Dodoma, ikiwa ni hatua ya kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa maji katika taasisi hizo.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya mradi wa Kimaghai A, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Ally Akida, amesema mradi huo utawanufaisha zaidi ya watu 600 kwa kutatua changamoto ya muda mrefu ya maji katika eneo hilo.

Naye Kaimu Afisa Elimu wa Jiji la Dodoma, Yasin Mponda, ameishukuru PSSSF kwa kuitikia ombi la Shule ya Msingi Uhuru, akisema utekelezaji wa mradi huo umeifanya shule hiyo kujiona inathaminiwa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru, Agatha Mosha, amesema upatikanaji wa maji umewezesha shule hiyo kuanzisha bustani ya mbogamboga kwa ajili ya kuboresha lishe ya wanafunzi.

Amesema mradi huo unatarajiwa kunufaisha zaidi ya watu 500, huku uwepo wa maji ukiwawezesha wanafunzi kupata mazingira bora ya kujifunzia na kushiriki shughuli za kilimo cha mbogamboga.

Makabidhiano ya miradi hiyo yamefanyika Novemba 3 na 4, 2026, yakiongozwa na Meneja wa PSSSF Kanda ya Kati, Lulyaya Sayi, aliyewataka wanafunzi, walimu na wananchi kutunza visima pamoja na miundombinu yake ili iendelee kutoa huduma kwa muda mrefu.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments