Sunday, November 9, 2025
spot_img
HomeBiasharaWatanzania kicheko malipo kidigitali kupitia Mixx 'Nyama Choma Festival'

Watanzania kicheko malipo kidigitali kupitia Mixx ‘Nyama Choma Festival’

Dar es Salaam, 06 Septemba 2025 – Maelfu ya Watanzania waliokusanyika katika viwanja vya Leaders kufurahia tamasha la ‘Nyama Choma Festival’ wameridhishwa na huduma ya malipo kidigitali iliyotolewa na Mixx wakisema imeondoa adha kubwa ya utafutaji wa chenji na kufanya maisha kuwa rahisi.

Wakizungumza na waandishi wa habari, baadhi ya washiriki walisema mfumo huu umefanya malipo kuwa haraka na salama, huku wakifurahia burudani, chakula kitamu, na muziki wa moja kwa moja.

Steve Elias, mkazi wa Kinondoni, alisema: “Nimefurahi kwakweli leo nimenunua vinywaji na nyama bila kusumbuana na watoa huduma. Malipo yote nimefanya kupitia Mixx. Malipo yamefanyika haraka bila foleni wala usumbufu wowote. Naye Mwajuma Aziz, mkazi wa Kigamboni, aliishukuru Mixx kwa kuendelea kuja na masuluhisho ya kidigitali ambayo yanarahisisha maisha ya Watanzania.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments