Tuesday, May 5, 2026
spot_img
HomeHabariWaziri Kombo amwakilisha Rais Samia CHOGM

Waziri Kombo amwakilisha Rais Samia CHOGM

Kati ya mambo muhimu katika mkutano huo ni pamoja na kumchagua Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola. Masuala mengine nyeti yatakayojadiliwa ni pamoja na uwekezaji, kutafuta suluhu ya pamoja kwa ajili ya maendeleo endelevu, mabadiliko ya tabianchi, usawa wa kijinsia, uchumi, demokrasia, na amani.

Mkutano huu utaibua changamoto na matarajio ya wanachama, huku Tanzania kama moja ya wanachama 56 wa Jumuiya ya Madola ikiwa miongoni mwa wale watakaonufaika katika sekta za uwekezaji, mabadiliko ya tabianchi, uchumi stahimilivu, na kubadilishana ujuzi kati ya mafanikio mengine mengi.

Kombo amewasili Samoa na kupokelewa na Waziri wa Fedha wa Samoa Mhe. Lautimuia VaÊ»ai. Akiwa safarini  Mhe. Kombo amefanikiwa kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Antigua na Barbuda,  Gaston Browne pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Utalii wa Seychelles, Sylvestre Radegonde.

Kaulimbiu ya mkutano wa mwaka huu ni Ustahimilivu katika kufikia malengo ya pamoja ya kimaendeleo ‘One Resilient Common Future: Transforming Our Common Wealth’.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments