HomeElimuWanafunzi 198 waelekea China, 189 India

Wanafunzi 198 waelekea China, 189 India

📍Wapatiwa Pasipoti, visa, tiketi na nyaraka nyingine muhimu za safari

📍Mollel ataka wanafunzi 387 wanaoelekea China, India kuchungulia fursa za biashara

📍GEL yawafungulia milango fursa za elimu duniani wanafunzi 387, waenda India na China

GLOBAL Education Link (GEL) imewakabidhi nyaraka rasmi za safari wanafunzi 387 wa Kitanzania wanaotarajia kwenda kuendelea na masomo ya elimu ya juu nchini China na India, huku wakihimizwa kutumia fursa hiyo kupata zaidi ya shahada kwa kujenga maarifa, ujuzi, teknolojia, mitandao ya kimataifa na uwezo wa kujitengenezea fursa za maisha.

Ukabidhi huo umefanyika kupitia mikutano miwili maalumu iliyofanyika Agosti 10 na 11, 2026 katika Ukumbi Mkuu wa Makao Makuu ya Global Education Link, Dar es Salaam, na kuhudhuriwa pia na wazazi na walezi wa wanafunzi hao.

Kati ya wanafunzi hao, 198 wanaelekea nchini China na 189 wanaelekea nchini India kwa ajili ya kuanza masomo katika vyuo mbalimbali vya elimu ya juu.

Wazazi na walezi waliohudhuria mikutano hiyo kwa ajili ya kushuhudia ukabidhi wa nyaraka na kupata maelekezo kuhusu safari na maisha ya watoto wao watakapokuwa nje ya nchi.

Lengo kuu la mikutano hiyo lilikuwa kuwakabidhi wanafunzi nyaraka muhimu za safari ambazo zimekamilishwa na GEL kama sehemu ya huduma inayofanywa nataasisi hiyo katika hatua mbalimbali za maandalizi yao, zikiwemo pasipoti, visa, tiketi za ndege, NOC (No Objection Certificate), cheti au kijitabu cha chanjo ya homa ya manjano (Yellow Fever Certificate) pamoja na nyaraka nyingine zinazohitajika na mamlaka husika kulingana na nchi, chuo na masharti ya safari ya mwanafunzi katika chuo husika.

Mbali na kukabidhiwa nyaraka hizo, wanafunzi pamoja na wazazi na walezi wao walipata maelekezo ya mwisho kuhusu taratibu za safari, uhamiaji, mazingira ya vyuo, makazi, bima ya afya, usalama, matumizi ya fedha, nidhamu na namna ya kukabiliana na mazingira mapya watakapofika katika nchi wanazokwenda.

Mtoa mada mkuu katika mikutano hiyo alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link, Bw. Abdulmalik Mollel, akishirikiana na wawakilishi wa vyuo kutoka China na India waliotoa ufafanuzi kuhusu masomo, huduma za vyuo na maisha ya mwanafunzi wa kimataifa.

Global Education Link ni wakala wa vyuo vikuu vya nje ya nchi mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 19 katika kusaidia wanafunzi wa Kitanzania pamoja na wazazi na walezi wenye watoto wenye ndoto ya kupata elimu ya juu nje ya nchi.

Katika kipindi hicho, taasisi hiyo imekuwa ikitoa mwongozo katika hatua mbalimbali kuanzia ushauri wa kielimu, uchaguzi wa programu na chuo, maombi ya udahili, maandalizi ya nyaraka, visa, safari na maandalizi ya mwanafunzi kabla ya kuondoka nchini.

Akizungumza katika mikutano hiyo, Mollel aliwataka wanafunzi kutokwenda China na India kwa lengo la kupata cheti au shahada pekee, bali kutumia mazingira ya vyuo watakavyosoma kujenga uwezo mpana utakaowasaidia baada ya kuhitimu.

Alisema kwenda kusoma nje ya nchi kunamfungulia mwanafunzi mazingira mapya yenye teknolojia, maabara, warsha, vituo vya ubunifu, wataalamu pamoja na wanafunzi kutoka mataifa mbalimbali, hivyo ni jukumu la mwanafunzi mwenyewe kutumia fursa hizo kwa manufaa yake na Taifa.

Aliwataka vijana hao kwenda zaidi ya masomo yao ya darasani kwa kutembelea maabara, warsha na vituo vya ubunifu na kujifunza kwa vitendo namna teknolojia na bidhaa mbalimbali zinavyozalishwa na kutumika katika kutatua changamoto za jamii.

Akitolea mfano mwanafunzi anayesomea Business Administration, alisema haipaswi kutosha kujifunza nadharia za usimamizi wa biashara pekee, bali mwanafunzi huyo anapaswa kutafuta maarifa kuhusu bidhaa, teknolojia, uzalishaji na mifumo mbalimbali ya viwanda ili aweze kuelewa kile anachoweza kukisimamia au kukigeuza kuwa biashara.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments